script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X
NJIA RAHISI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA KUKU WAKO (LAYERS NA BROILERS)

Habari Ndugu Mfugaji,
Karibu katika muendelezo wa mfululizo wa mafunzo ya ufugaji wa kuku kutoka Mshindo media

Mshindo media dhamira yetu ni kuhakikisha UNAFANIKIWA  KUPITIA UFUGAJI  hapa  Ufugaji na matibabu Vet

Leo Tutazungumzia Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Mayai

( LAYERS na KUROILERS )
Utengenezaji wa chakula cha kuku kwa kutumia
Formula sahihi ni njia nzuri kwa mfugaji kwa kupunguza gharama za mradi wake, pia kuhakikisha chakula kinakua na virutubisho muhimu kwa usahihi.
Ifuatayo ni formula ya utengenezaji wa chakula cha Kuku, Starter, grower na Finisher.
------------------------------
1. CHICKS STARTER , WIKI 1 - 5
• Pumba za maindi 41kg
• Dagaa walio sagwa 5kg
• Mtama ulio sagwa 25kg
• Mashudu ya alizeti 22kg
• Chumvi 0.5kg
• Damu iliyo sagwa 3kg
• Unga wa mifupa 2kg

• Methionine 0.25kg
• Prexix 0.5kg
• Vitamins 0.5kg
• Lysine 0.25kg
TOTAL =100KG
------------------------------
GROWER MASH, WIKI 6 - 16
• Mashudu ya alizeti 22kg
• Ngano nzima 5kg
• Dagaa walio sagwa 11kg
• DCP 1kg
• Unga wa mifupa 5kg
• Chokaa 2kg
• Chumvi 0.5kg
• Mahindi yaliyo parazwa 10kg
• Premix  0.5kg
TOTAL =100KG
------------------------------
LAYERS MASH WIKI 17
• Mashudu ya alizeti 20kg
• Pumba za mahindi 35kg
• Chokaa 3kg
• Mtama 6kg
• Dagaa walio sagwa 12kg
• Unga wa mifupa 5kg
• Damu iliyo sagwa 5kg
------------------------------
MUHIMU
- Hakikisha unachanganya  vizuri ili kupata mchanganyiko wenye uwiano Sahihi wa virutubisho.
- Chakula kihifadhiwe vizuri kuzuia unyevu.
- Kuku wapewe chakula kwa kiasi kulingana na umri na idadi yao
Ahsante kwa Kutumia Huduma zetu!
............................................................................................................................

2 comments:

Unknown said... March 21, 2021 at 1:34 PM

Hiyo growermash na finisher haijatimia ujazo wa kilo mia 100kg kunavitu vingine malizia hapo👍

Unknown said... March 21, 2021 at 1:35 PM

Hiyo growermash na finisher haijatimia ujazo wa kilo mia 100kg kunavitu vingine malizia hapo��

 
Top