
Kupungua kwa mayai yanayo zalishwa kwa siku katika shamba lako la kuku watagao mayai ni dalili moja wapo inayo onesha kwamba kunatatizo katika kundi lako la kuku. Kulingana na utafiti ulio fanywa na shirika la FAO una onesha kwamba kwa kawaida kuku aliye fikia umri wa miezi mitano au sita nakuendelea inatakiwa atage yai moja kila baada ya saa 24 hadi 26, kwa maana hiyo kila siku kuku wako inatakiwa atage yai moja.
Kama
vile tunavyo kuwa makini kufuatilia kinyesi cha kuku kugundua kama kuku
anaumwa au anatatizo vivyo hivyo tunapaswa kufuatilia uzalishaji wa
mayai kwa siku. Mabadiliko katika uzalishaji wa mayai yanaweza
kusababishwa na magonjwa, mabadiliko ya tabia, mazingira na stress.
Ilikujua sababu haswa inayo badilisha uzalishaji wa mayai katika kundi
lako la kuku (flock) ina takiwa urejee na ukague historia ya kundi lako
na pia ukague hali ya kuku wote(physical assessment) huku ukijiuliza
maswali yafutayo;-
· Je kuna kuku wapya au
wageni umewaongeza kwenye kundi lako?, kwasababu kuku wageni huweza kuwa
chanzo cha kuleta magonjwa kama sehemu walio toka kuna mlipuko wa
ugonjwa.
· Je kuna mabadiliko yoyote katika aina
ya chakula unachowalisha, mabadiliko ya makazi (banda) au mpangilio
ndani ya banda, mabadiliko ya hali ya hewa, masaa ya mwanga na giza,
mabadiliko kwenye kinyesi?.
· Je kunadalili
yoyote ya uwepo wa wanyama walao mayai au kuku (predators) au magonjwa
ya kuku?. Kunawakati mwingine unaweza dhani kwamba kuku hatagi kumbe
sivyo ila kuna wanyama kama paka, mbwa na vicheche wanakula mayai bila
wewe kujua.
1. KUPUNGUA KWA MASAA YA MWANGA (LIGHTING).
Mwanga husisimua “pituitary gland”kwenye
kuku ili kuchochea uzalishaji wa mayai. Mtiririko mzuri wa utagaji wa
mayai kwa kuku huhitaji masaa 14 mpaka 16 ya mwanga, kwa mfano kuna
baadhi ya majira ya mwaka ambapo jua huwahi kuzama na kuchelewa
kuchomoza hivyo husababisha masaa ya mwanga kuwa machache kwa siku,
hivyo huathili uzalishaji wa mayai kwa kuku.
Ili kuondoa
tatizo hili la upungufu wa masaa ya mwanga unaweza kuweka taa za
umeme(artificial light) ndani ya banda lako la kuku wa mayai na uziwashe
baada tu ya giza kuingia kwa masaa mawili hadi matatu. Kutokana na
utafiti uliofanywa na shirika la FAO una onesha kwamba kuwapa kuku wako
mwanga kwa msaa mawili hadi matatu huweza kuimalisha utagaji wa mayai
kwa asilimia 20 hadi 30, hii inaonesha ni jinsi gani mwanga ni muhimu
sana kwa kuku wa mayai.
2. STRESS NA MABADILIKO MBALIMBALI.
Ni
rahisi sana kwa kuku kuathirika na stress na hii hupelekea kupunguza
utagaji wa mayai, kwa kawaida kuku hapendi mabadiliko, yanaweza kuwa
mabadiliko ya chakula, mpangilio wa vyombo vya chakula na maji ndani ya
banda na kuwa hamisha kwenda banda jingine, pia stress inaweza
sababishwa mambo kama kusumbuliwa na minyoo, kupe, viroboto, na chawa,
joto kari, kelele za wanyama kama mbwa au paka, kelele za machine au
magari zisizo isha, yote hayo yanaweza sababisha stress kwa kuku na
hatimaye kuathili utagaji wa mayai.
3. MAGONJWA.
Kuku
anapo shambuliwa na magonjwa mara nyingi hudhoofu na kukosa nguvu
mwilini pia hupoteza hamu ya kula, katika wkati kama huu kuku hupunguza
utagaji au kusismisha kabisa utagaji kutegemeana na namna ugonjwa ulivyo
muathili. Kuepuka matatizo haya hakikisha kwamnba kuku wanapewa chanzo
zote wanazo stahili, watibu kwa wakati pale wanapo ugua na pia jitahidi
sana kuzuia vyanzo vya magonjwa ambavyo vipo ndani uwezo wako kama
mfugaji.
4. UMRI WA KUKU
Kwa
kawaida kuku anapo fikisha umri wa miaka miwili uzalishaji wake wa mayai
hupungua, jinsi anavyo zidi kuwa na umri mkubwa uzalishaji wa mayai
hupungua lakini huwa wanataga mayai makubwa kiumbo kuliko kuku wadogo.
Ili kuongeza faida na ufanishi katika mradi wako hakikisha kwamba
unaondoa kuku walio zeka na kuwaleta wengine ambao hawajazeka, kwasababu
hao kuku wazee wanaweza wakawa wanakula chakula kingi lakini hawatagi
hivyo husababisha hasara ndani ya shamba.
5. UKOSEFU WA MAJI
Upatikanaji
wa maji safi na salama ni wa muhimu sana katika mfumo wa kutengeneza
mayai kwa kuku. Uzalisha wa mayai huathirika endapo kuku wako
hawatakunywa maji ya kutosha pengine kwa sababu ni machafu, hayajawekwa
mahala ambapo panafikika vizuri hivyo kuku wanashindwa kunywa kiurahisi
au hayana radha halisi ya maji kutokana uchafu au vitu ambavyo
vimechanganywa ndani yake. Hakikisha kwamba maji safi na salma
yanapatikana ndani ya banda muda wote na yaweke mahali ambapo panafikika
na pia hakikisha kwamba idadi ya vyombo vya maji ina kidhi mahitaji
kulingana na idadi ya kuku wako.
6. JOTO (TEMPERATURE).
Mtiririko
wa utagaji wa mayai kwa kuku waweza athiriwa na joto katika mazingira
husika. Kwa kawaida ili kuku aendele kutaga katika mtiririko wake wa
kawaida yani yai moja kila siku anahitaji joto lisiwe chini ya 11oC na lisiwe zaidi 28oc .
Jedwali apo chini lina onesha matokea ya viwango tofauti tofauti vya joto kwa kuku wako katika uzalishaji.
7. MATATIZO KATIKA MFUMO WA UZAZI
Magojwa
au kasoro za kimaumbile katika mfumo wa uzazi pia zaweza sababisha
kushuka kwa utagaji wa mayai, kwahiyo hakikisha kwamba kuku wako wa
mayai hana matatizo ya kimaumbile. Tafuta msaada wa dakitari wa mifugo
kama kuku ata onekana kuwa amevimba au ametuna kama mfano wa puto lenye
maji upande wa chini wa tumbo au unaweza ona kama kuna dalili ya yai
kukwama .
8. UPUNGUFU WA VIRUTUBISHO.
Upungufu
wa virutubisho muhimu katika chakula cha kuku wa mayai husababish
kupungua kwa uzalishaji wa mayai. Hakikisha kwamba kuku wako wanapewa
chakula ambacho kina virutubisho vyote ambavyo ni vya muhimu kwake. Ili
kuondoa tatizo hili unaweza kununua chakula kutoka madukani ambacho
kimeshafanyiwa mchanganyiko maalumu wa virutubisho vinavyo faa kwa kuku
wa mayai au ilikupunguza ghalama unaweza kujifunza fomula mbalimbali za
mchanganyiko wa chakula na ukatengeneza chakula chako mwenyewe kwajili
ya kuku wako. Katika chakula hicho cha kukuk wa mayai hakikisha kwamba
kuna kiwango cha kutosha cha protini, madini kashiamu na wanga.
9. KUPUKUTISHA MANYOYA (MOLTING).
Hii
ni tabia ya asili ambayo hutokea kwa kuku katika hatua mbailimbali ya
ukuaji, baadhi ya kuku wanawza kupukutisha manyoya mengi kwa wakati
mmoja na akabaki wazi baadhi ya sehemu za mwili wake kama mgongo na
shingo au akapukutisha manyoya yake kidokidogo huku mengine yakiota,
ambapo haitakuwa rahisi kwa wewe kugundua kama yupo katika hatua hii ya
kupukutisha manyoya.
Katika kipindi hiki kuku hupunguza
au kusimamisha kabisa utagaji, hii hutokana na ukweli kwamba kipindi
hiki kuku hutumia protini nyingi na nguvu nyingi kuotesha manyoya mapya
mwilini mwake kuliko kuzalisha mayai. Hali hii ni ya asili na haizuiliki
kinacho takiwa katika kipindi hiki ni kujitahidi kumpa chakula ambacho
ni bora(balanced diet).
10. HALI YA KUATAMIA.
Hi
ni hali ya kuku kulalia mayai yake ili kuyapa joto na kuruhusu ukuaji
wa kiini tete (embryo) ndani ya yai. Hali hii ni kawaida kwa kuku wetu
wa asili. Kuku anapo anza kuatamia huacha kutaga mayai, pia kama kuku
huyu anaye atamia yupo ndani ya banda ambalo kuku wengine bado
wanaendelea kutaga, hupelekea kuku wengine kupatwa na hali hii pale tu
wanapo muona ka atamia. Kwahiyo ni vyema kuku wanao atamia wasikae kweny
banda moja na wale wanao endelea kutaga.
ZINGATIA:
ILI KUONA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA MAYAI KWA KUKU WAKO NI
VYEMA UKACHUKUA HATUA YA KUSHUGHULIKIA VIZUIZI VYOTE HAPO JUU.
USICHAGUE TATIZO MOJA LA KUTATUA HAKIKISHA UNA YA TATUA YOTE KWA WAKATI
NDIPO UTAKAPO ONA MATOKEA MAZURI.
......................................................................................................
0 comments:
Post a Comment