Katika kipengele muhimu ambacho mfugaji hapaswi kukipuuza ni chanjo kwa kuku, Kwani chanjo huongeza kinga ya kuku kupambana na vimelea vya ugonjwa husika kabla haujaanza kushambulia kuku
Zipo chanjo za aina tofauti tofauti ambazo zimegawanyika katika makundi,
Live vaccine
, hizi ni zile ambazo hutumia vimelea hai vilivyo pumbazwa (*In active*) vya magonjwa mfn Virus husika wa magonjwa kama
Newcastle Disease Vaccine (Chanjo ya Kideri),
Infectious Bronchitis vaccine,
Infectious Bursal Disease Vaccine (Chanjo ya Gumboro),
Fowl Pox Vaccine (Chanjo ya ndui).
Kuna baadhi ya chanjo huwa ni adimu sana kupatikana ,
Kama
Chanjo ya Salmonella
Chanjo ya Corryza
Chanjo ya MG
ila kwa urahisi unaweza kuwatafuta *ZOETIS* au *CEVA*, na makampuni mengine ya madawa ya mifugo huwa niwasambazaji na wauzaji wakubwa wa chanjo za mifugo.
Vitu vya kuzingatia , Kabla, wakati na baada ya chanjo.
Kuku hapaswi kuwa mgonjwa.
Kuku hapaswi kuwa kwenye dozi ya dawa.
Usafi wa vyombo vya kuchanjia.
Kusoma Expire date na Batch namba
Dose ya chanjo(500,1000,5000) usikariri kwamba chanjo zinafanana ujazo.
Umri wa kuku, uwiane na aina ya chanjo.
Chanjo zizingatie cold chain, yaani zihifadhiwe katika hali ya ubaridi na kutolewa pale tu itakapo kua inatumika kwa chanjo
NB: LIVE VACCINE USIBADILISHE RATIBA.
Ratiba za chanjo zinatofautiana kutokana na aina ya kuku
Kwa kuku wanaotaga (Layers, Chotara, kienyeji) mfumo wao wa chanjo kitaalamu na kwa maelekezo ya miongozo mingi ya chanjo
- Siku ya kwanza Marek’s Vaccine.
- Siku ya 7 Newcastle Vaccine/kideri
- Siku ya 14 Gumboro, Infectious Bursal Disease Vaccine
- Siku ya 21 Newcastle Vaccine (kideri).
- Siku ya 28 Gumboro, Infectious Bursal disease.
Siku ya 30 Fowl Pox Vaccine (chanjo ya ndui). Usiipuuze japo ni gharama kati ya (15000-18000).
Rudia Newcastle Vaccine kila baada ya miezi mitatu.
Kwa kuku wa nyama, *(Broilers)*
Mfumo wa kwanza
- Siku ya 7 chanjo ya Newcastle/kideri.
- Siku ya 14 Gumboro
- Siku ya 21 Gumboro
Mfumo wa pili
Siku ya 7 newcastle /kideri
Siku ya 14 Gumboro/Infectious Bursal Disease
Siku ya 21 Newcastle/kideri
MFUMO WA UCHANJAJI.
Kwa chanjo za maji,
Safisha vyombo vya maji
Wape kuku chakula, na uondoe maji kwa masaa mawili kabla ya kuweka maji ya chanjo
Andaa maji ya chanjo, kwa Kuchemsha, au Kuweka dawa ya kuondoa Chlorine (Cevemune-Chlorex blue) yakae dakika 15
Changanya chanjo kwa kuzingatia dozi ya chanjo kwa uwiano wa idadi ya kuku.
Wape kuku chanjo na maji ya chanjo yakae masaa mawili kisha yaondoe na uwape maji yasiyo na chanjo (unaweza kuweka vitamins baada ya kutoa maji ya chanjo).
Chupa za chanjo, maji ya chanjo yaliyobaki yamwagwe/ kutupwa mbali na mazingira ya banda la kuku.
Kwa chanjo zinazohitaji usimamizi kama chanjo ya *Ndui* na zote za *Inactive vaccine* Nivema ifanywe na Daktari wa mifugo, au Chini ya usimamizi wa Daktari wa mifugo.
NB: Mara nyingi chanjo hufanywa kwa interval ya siku 7 hasa zile za mfumo wa chakula ili kuruhusu mwili kuimarisha kinga ya ugonjwa husika kabla ya kuanza kuandaa tena ya ugonjwa mwingine
Pia mantiki ya kurudia chanjo ya pili huwa ni kuimarisha ile kinga iliyo wekwa na chanjo ya awali ili kumkinga kuku kwa kipindi kirefu zaidi
RATIBA ZA CHANJO*
Kuku wanaokaa muda mrefu kama Wa MAYAI, CHOTARA, KIENYEJI
- Siku ya 1 chanjo Marek’s
- Siku ya 7 chanjo ya Newcastle/kideli
- Siku ya 14 chanjo ya gumboro
- Siku ya 21 chanjo ya kideli/Newcastle
- Siku ya 28 chanjo ya gumboro
- Siku ya 30 chanjo ya ndui
Baada ya miezi mitatu dawa za minyoo
Rudia chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatu
KWA KUKU WA NYAMA/ BROILER*
Hawachanjwi mareks
Siku ya 7 chanjo ya Newcastle
Siku ya 14 chanjo ya gumboro
Siku ya 21 chanjo ya kideli
Wafugaji wengi wamekua wakichanja hivyo kwakua huuza kuku ndani ya siku 28-30
Kama utauza kuku baada ya siku 40 chanja chanjo ya gumboro siku ya 28.
*Kumbuka*
Chanjo zote zamaji zinatakiwa zikae ndani ya muda wa saa 1-2…baada ya hapo mwaga maji OSHA vyombo na badilisha maji ya kawaida
Zingatia usafi wa maji na vyombo kabla na baada ya chanjo
Kama utatumia maji ya mvua au usiyoamini kuwa ni masafi kwajili yachanjo yatibu kwa kidonge kinaitwa CEVAMUNE/Chlorex blue.
Nimependa tujifunze hayo kwa leo nawatakia ufugaji mwema
.......................................................
0 comments:
Post a Comment