script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X
https://www.mshindoveterinarycentre.com/2021/02/sifa-za-kuku-wa-asili-faida-na.html
 
SIFA ZA KUKU WA ASILI.
● Wastahamilivu wa magonjwa, lakini ni muhimu wakikingwa kutokana na magonjwa ya kuku kama vile mdondo, ndui ya kuku n.k. ili kuweza kuwaendeleza. 
● Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini, lakini ili kuwaendeleza ni lazima kuwapa chakula cha ziada.
● Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa, kulea vifaranga na ustahamilivu wa mazingira magumu (ukame, baridi n.k)
● Nyama na mayai yake yana ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa hivyo vina bei kubwa.
● Kwa kiasi fulani wana uwezo wa kujilinda na maadui kama vile mwewe.

FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI.
● Chakula-- nyama ya kuku wa asili na mayai hutumika kama chakula muhimu cha binaadamu chenye protini.
● Chanzo cha kipato-- mfugaji hupata fedha akiuza kuku na mayai.
● Chanzo cha ajira-- ufugaji wa kuku hutoa ajira kwa jamii.
● Kuku wa asili hutumika kwenye shughuli za ndoa kama vile kutoa mahari na pia kitoweo muhimu katika sherehe.
● Gharama za kuanzisha na kuendesha mradi huu.
● Ni kitoweo rahisi na chepesi kwa wageni kuliko wanyama wakubwa kama ng'ombe au mbuzi.
Soko lipo la uhakika ukilinganisha na kuku wa kisasa kwani nyama na mayai yake hupendwa zaidi na walaji.

MIFUMO YA UFUGAJI KUKU WA ASILI ( KIENYEJI )
Ipo mifumo mitatu ya ufugaji wa kuku wa asili inayotumika nchini Tanzania. Mifumo hiyo ni:
● Ugaji huria.
● Ufugaji wa nusu huria.
● Ufugaji wa ndani.

UFUGAJI HURIA.
Kuku huachiwa wenyewe katika kujitafutia chakula na maji. Njia hii inatumika zaidi kufuga kuku wa kienyeji. Mara chache sana mfugaji huwapatia kuku chakula cha ziada. Kwa ufugaji huu lazima kuwe na eneo kubwa la kutosha kuku kuzunguka na kujitafutia chakula.

FAIDA ZA UFUGAJI HURIA.
● Ni njia rahisi ya kufuga.
● Gharama zake pia ni ndogo.
● Kuku wanapata mazoezi ya kutosha.
● Kuku wanapata chakula mchanganyiko ambacho kinafaa kiafya.
Hasara za ufugaji huria.
● Kuku huwa hatarini kuibiwa au kudhurika na wanyama wakali na hali mbaya ya hewa.
● Ukuaji wa kuku una kuwa hafifu, hufikia uzito wa kilo 1.2 baada ya mwaka.
● Ni rahisi kuambukizwa magonjwa.

KUFUGA NUSU NDANI-NUSU NJE.
Huu ni mtindo wa kufuga ambapo kuku wanakuwa na banda lililounganishwa na uzio kwa upande wa mbele. Hapa kuku wanaweza kushinda ndani ya banda wakiwa ndani ya uzio.
● Wakati wa mchana kuku wanakuwa huru kushinda ndani ya banda hasa wanapotaka kutaga na wakati wa kuatamia au wanaweza kukaa ndani ya uzio nje.
Faida za kufuga nusu ndani nusu nje.
● Kuku wanakuwa salama mbali na maaduni kama mwewe n.k.
● Utaweza kuwalisha kuku wako vizuri hivyo wataweza kuongeza uzalishaji wa mayai, kuongezeka kilo na watakua haraka.
● Itakuwa rahisi kwako kudhibiti wadudu na vimelea vinavyoweza kuleta magonjwa kwa kuku wako.
● Ni rahisi kuwatenganisha kuku katika makundi tofauti na kuwahudumia ipasavyo.
● Ni rahisi kutambua kuku wagonjwa kuliko kufuga huria.
● Kuku watapata mwanga wa jua wa kutosha pamoja na hewa safi. Wakati wa jua kali watakuwa huru kuingia ndani ya banda na kukaa kivulini.

KUFUGA NDANI YA BANDA TU.
Njia nyingine ni kuwafuga kuku ndani ya banda tu. Katika njia hii kuku hukaa ndani wakati wote. Njia hii ya ufugaji hutumiwa zaidi na wafugaji wa kuku wa kisasa. Lakini yaweza kuyumika hata kwa kuku wa kienyeji hasa katika sehemu yenye uhaba wa eneo.
Changamoto za ugaji wa ndani ya banda tu.
● Unatakiwa uwe na muda wa kutosha wa kuwahudumia kuku wako kikamilifu.
● Pia unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa wa kujenga banda na kuwanunulia chakula.
● Ugonjwa ukiingia ni rahisi kuambikizana. Vilevile kuku huanza tabia mbaya ya kudonoana n.k.
Faida za kufuga ndani tu.
● Ni rahisi kutambua na kudhibiti magonjwa.
● Ni rahisi kudhibiti upotevu wa kuku, mayai na vifaranga.
● Ni rahisi kuwapatia chakula kulingana na mahitaji ya kila kundi.

NI UFUGAJI UPI UNAFAA ZAIDI ?
● Kwa ujumla, njia rahisi na inayopendekezwa kutumiwa na mfugaji wa kawaida ni ya ufugaji wa nusu ndani nusu nje, yaani nusu huria. Hii inatokana na faida zake kama zilivyoainishwa hapo
........................................................................................................................................

0 comments:

 
Top