script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X

Nawasalimu kwa jina la yeye anitiae nguvu anilinda na alienipa kibali hiki naamini muwazima na wenyeafya njema 

Leo tuangalie chanjo za asili kwanzia siku moja na kuendelea pia baadhi zaweza kuwa kinga  kuwa tiba kabisa kwa ugonjwa 

Basi tuanze somo letu la leo kwa jina la muumba mbingu na nchi MUNGU mwenyezi.

Siki 1 
       Kuku wapewe majani ya #mlonge najani ya #mpapai #Mkaa na #Aloe_vera.
Mitishamba hii hukinga #Ndui #Kuhara_damu #Kuhara_choo_cheupe na #Kipindupindu_cha_kuku 
Saga mkaa weka kwenye vijiko 10 kwa maji ya lita moja na nusu majani ya papai aloe vera mlonge twanga twanga kisha wape ila usichanganye dawa hizi kila daw na wakat wake 

        Siku 7 
Kuku wapewe #Ndulele  ni kinga ya #Ini #Typhoid tanga majani viganja 5  kwa lita moja na nusu 

        Siku 14 
Kuku wapewe majani ya #Mpapai hutibu na kukinga #Minyoo 
Mara hii chemsha majani kisha wape 

          Siku 21
Kuku wapewe #Mwarobaini hukinga na kutibu #Vidonda #Kuhara na #Mafua_ya_kawida
Twanga majani viganja 4 kwa lita moja ya maji loeka kisha wape 
  
     Siku 28
Kuku wapewe #Pilipili_kichaa #Kutunguu_saumu #Majivu na #Katani 
Hukinga na kutibu  #Mafua_Makali 
 Twanga pilipili kichaa 5 changanya na maji yenye majivu vijiko 3 maji nusu lita kisha wape ila kitunguu saumu na katani usichanganye 

           Siku 35
Kuku wapewe #Aloe_vera #Ndulele na #Katani
Kinga ya #Newcastle 
Twaga majani ya ndulele Aloe vera na katani ila usichanganye katani matawi 2 kwa lita 1 ya maji ndulele viganja 5 kwa lita moja na nusu
         
         Siku 42 
Kuku wape majani ya #Muembe #Mkaa #Mtalangonyo hukinga Gumboro Kideri 
Mkaa usage kisha weka vijiko 10 kwa lita moja majani ya muembe viganja 3 kwa lita moja na nusu 

        Siku 49 
Anza kuludia chanjo hizi pia zingatia usafi na chakula bora kwa kuku wako hutopata kuku anaeumwa hata mmoja 
.....................................................

0 comments:

 
Top