script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X
UFUGAJI  WA BATA MZINGA NA MBINU ZA UFUGAJI BORA
UFUGAJI WA BATA MZINGA

UFUGAJI BORA WA BATA MZINGA (Meleagris gallopavo) : Ulaji wa nyama ya bata mzinga umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni na kitoweo chake kimezoeleka kuliwa wakati wa sikukuu mbalimbali kama Idd mbarak, Krismasi na Pasaka.

Asili yake ni Amerika ya kati ambako walitokana na bata mzinga pori/mwitu. Bata mzinga wengi wanaofugwa ni machotara, yaani waliotokana na aina kama wale weupe wa kutoka Uholanzi na Beltsville, wenye rangi ya shaba. Uzito wa bata mzinga dume wale  wakubwa ni kilo 11-14 na majike ni kilo 7 hadi 8 wakiwa hai. Wale aina ndogo madume huwa na kg 7-8 na majike kilo 4-5.

Kwa ujumla ufugaji wa bata mzinga unaendelea kukua sasa hivi kuliko ulivyokuwa hapo awali.

 

UZALISHAJI:

Madume na majike wanabalehe kwa wakati mmoja ambao ni umri wa mwaka mmoja ambapo huanza kupandana lakini huwa hawajakomaa. Ifikapo umri wa miaka mitatu ndipo majike huweza kutaga mayai ambayo yanaweza kuanguliwa, endapo dume la umri huo atakuwa anapanda majike ya kisasa yenye uwezo wa kutaga mayai 90 kwa mwaka. Lakini wale wa kienyeji ni mayai 20 tu kwa mwaka,

‡ Madume huwa na maumbo makubwa kuliko majike na mara nyingi huwaumiza majike kwa makucha ya miguuni katika harakati za kuwapanda. Hivyo tunashauriwa kupunguza hayo makucha.

‡ Dume mmoja hutosha kupandisha majike 10 japokuwa yana tabia ya kuchagua majike, na mpando mmoja unaweza kurutubisha mayai yote yanayozalishwa na majike. Majike hayatarajiwi kumkosa dume zaidi ya wiki tatu ili mayai yaweze kuanguliwa. Vinginevyo mayai yanaweza kukosa virutubisho.

‡ Majike yana kawaida ya kujitengenezea viota vyao kwa ajili ya kutagia, lakini pia mfugaji anaweza kuwatengenezea.

‡ Sehemu ya kuwapandishia majike huweza kutengenezwa kwa kujenga nguzo tatu mithili ya pembetatu na kuziziba pande mbili kutumia nyasi, magunia au mikeka.

‡ Usiweke zaidi ya dume moja kwenye kundi moja la majike kumi maana yana tabia ya kupigana.

‡ Madume yasiwe manene na vifua vipana sana maana yatashindwa kupanda kikamilifu.

‡ Mwanga wa taa ya umeme hufanya majike watage mayai mapema na mengi.

‡ Mayai yakapoatamiwa yasafishwe na dawa aina ya Potassium permanganate ambayo huua vijidudu vya magonjwa kwenye ganda la yai. Ni vyema kutumia dawa hii kwa mayai ya ndege wote wanaofugwa kabla ya kuatamiwa.

‡ Bata mzinga huatamia mayai kwa siku 28-32 na kuanguliwa siku ya 28-32.

‡ Kama mayai yatarutubishwa vyema na dume, na uatamaji wa jike kuwa mzuri, Vifaranga zaidi ya saba kati ya kumi  kuanguliwa.

Kuku anaweza kutumiwa kuangua mayai ya bata mzinga.

 

ULEAJI NA KUKUZA VIFARANGA

Uleaji na ukuzaji wa vifaranga ni kama ifanyikavyo kwenye kuku, isipokuwa bata mzinga huathiriwa sana na baridi na unyevunyevu. Vyanzo vya joto vitumike  kuongeza joto.

– Uleaji kwa wiki 4-5 unatosha, na hufanyike kama kwa kuku.

x Bata mzinga hukua haraka sana kuliko kuku kwa hiyo huhitaji nafasi mara mbili ya nafasi ya kuku.

x Wiki ya kwanza hadi ya nne watahitaji nafasi ya mita ya mraba 1 kwa vifaranga kumi

x Wiki ya 8 hadi 12 bata 6 mita 1 ya mraba.

AINA ZA BATA MZINGA
AINA ZA BATA MZINGA

x Wiki 4-8 bata mzinga 8 mita 1 ya mraba.

x Bata wakubwa 2 hutosha kwenye mita moja ya mraba.

x Joto katika uleaji liwe nyuzi 37.80C siku ya kwanza, mpaka 35.0C mwisho wa wiki ya kwanza. Baadaye huanza kupungua kwa 0.60C kila siku hadi joto la kawaida litakapohitajika.

x Wakiwa na umri wa miezi 4 wachaguliwe kwa aili ya kuwa madume na majike ya mbegu na wale watakaofugwa kwa ajili ya nyama (kuuzwa).

x Wale watakaochaguliwa kuwa wazazi walishwe vyakula vya asili ya mimea zaidi kuliko wale wa nyama kwa sababu chakula cha aina hiyo huwafanya wasinenepe sana, sifa ambayo haitakiwi katika kuwa wazazi.

x Haishauriwi kuwajaza katika nafasi ndogo maana watadonoana na kuambukizana magonjwa kwa urahisi.

 CHAKULA NA ULISHAJI

x Vifaranga vya bata mzinga huhitaji mwanga wa kutosha kwa ajili ya kuona maji na chakula kwa vile ni wagumu kuzoea chakula na maji, ikibidi waanzishe kwa kutumbukiza midomo yao kwenye vyombo vya chakula na maji.

x Vifaranga wapewe punje za nafaka zilizopondwa zikichanganywa na maziwa.

x Wape pia majani machanga, lakini yakatwe vipandevipande. Bata mzinga mmoja huhitaji wastani wa gramu 280 kwa siku.

x Vyombo vya chakula na maji visiwekwe kwenye sehemu zenye giza au mwanga mchache.

x Mahitaji ya chakula kama nafaka zilizopondwa kwa ajili ya kuwapa nguvu, mbegu za mafuta kuwapa joto, kunde, damu na dagaa kujenga mwili, vitamini na madini kulinda mwili, kuimarisha mifupa na mayai.

x Unaweza kupata vyakula hivyo kutoka kwenye maduka ya pembejeo za kilimo na mifugo pia kutoka viwanda vya kutengneza vyakula vya mifugo kama Quality Animal Feeds na Farmers Centre vilivyopo Amana –Ilala na wasambazaji wao mikoani.

 MAGONJWA:

Bata mzinga hushambuliwa zaidi na magonjwa yafuatayo;

– Black head

– Mycoplasmosis

– Ndui

BLACK HEAD/VICHWA VEUSI

x Ugonjwa huu unaojulikana zaidi kwa jina la ‘‘vichwa vyeusi’’ ndiyo unaowashambulia sana bata mzinga.

x Umri wa miezi 2-4 ndiyo hupatwa zaidi na dalili zinazojionyesha ni kutoa kinyesi cha rangi ya njano kila wakati ambacho hugandana kwenye manyoya ya mkiani. Vichwa huwa na rangi nyeusi, utumbo mdogo wenye sehemu mbili zinazofanana (Caeca) na maini huathirika kuwa rangi ya njano.

– Mabawa hushuka, manyoya huvurugika, macho huzubaa hayaoni na hufunga

– Kuku huwa na ugonjwa huu lakini hawaumwi

– Bata mzinga wakubwa huathirika kwa kiwango kidogo, kwa kuumwa kwa kipindi kirefu ukilinganisha na wale wadogo; baadaye huanza kukonda wanapokaribia kufa.

 TIBA

– Unaweza kutibu ugonjwa huu kwa kutumia dawa zenye mchanganyiko wa Tylosin, Sulphur, Trimethoprim/trimazine au tumia cotrim 480 WSP.

 MYCOPLASMOSIS; kama ilivoelezwa katika ukurasa uliopita.

 NDUI (FOWL POX)

Huu ni ugonjwa hatari sana kwa bata mzinga, husababishwa na virusi, mfugaji anashauriwa achanje mapema sana kati ya wiki ya 3 hadi
6, hii itasaidia bata wasipatwe na ugonjwa huu.

 DALILI:

Bata huonekana na vipele vya rangi ya kahawa (brown) au kijivu kwenye ngozi yake hasa katika upanga wa kichwa. Baada ya muda mfupi vipele hivi huwa vikubwa na kushikana, hatimaye hufanya majeraha makubwa yenye kutoa damu ukikata.

 TIBA:

Ugonjwa wowote unaosababishwa na virusi huwa hauna tiba, kinachotakiwa uwape dawa bata ili kuzuia magonjwa nyemelezi (prevent secondary infection).

Dawa zenyewe ni kama Neoxychick, au OTC plus au Oxyfarm 20% pamoja na vitamini mfano Farmvita au Stressvita

 

KINGA:

Bata wapewe Chanjo mapema, Wagonjwa wote watengwe kuzuia ugonjwa kuenea haraka.

Usafi ni jambo la kuzingatia zaidi,  Pulizia dawa V-RID ndani na nje ya banda.

 

MINYOO:

– Minyoo ya kwenye utumbo mdogo huwa na vijidudu na mayai ya ugonjwa huu kwa kuku.

– Kutokana na ugonjwa huu kuku watenganishwe na bata mzinga katika ufugaji.

– Dawa za minyoo zitumike kila baada ya miezi mitatu kama aina ya Piperazine na, Levamisole kupitia kwenye maji ya kunywa au chakula.

– Licha ya kuambukiza ugonjwa huu minyoo pia hunyonya damu na chakula cha bata mzinga na kusababisha kukonda na kukua polepole. Upungufu wa damu husababisha udhaifu hivyo kuambukizwa kirahisi na magonjwa mengine.

– Vilevile mfugaji anashauriwa kutumia dawa za kuangamiza wadudu washambuliao ngozi kama vile Akheri powder au dawa ya Ivemectin ambayo huangamiza minyoo tofauti kwa mkupuo.

Mfugaji pia anashauriwa kuwasiliana na wataalamu wa mifugo kwa ushauri wa masuala yote ya mifugo ambao utawapata
kwenye ofisi za serikali za kilimo na mifugo au kwenye maduka ya pembejeo na vituo vya mifugo.

.....................................................................................................................................

0 comments:

 
Top